Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmarck Production ya
jijini ambayo ndiyo inayaendesha shindano la Bongo Star Search (BSS)
hapa nchini Maadam Litah Paulsen amezungumza na wanahabari leo katika
ukumbi wa idara ya Maelezo juu ya maandalizi na utaratibu utakaotumika
kuendesha shindano hilo mwaka huu ambalo litashirikisha mikoa yote ya
Tanzania ambayo ni Dar es alaam, Arusha, Tanga, Kigoma, Tabora, Mwanza,
Mbeya, Iringa, Mtwara, Dodoma na Zanzibar na amesema shindano hilo
linatarajiwa kuanzia katika Jiji la Arusha tarehe 21 February, na
washiriki 48 wanatarajiwa kushiriki katika shindano hilo mara baada ya
mchujo wa washiriki wa mikoa yote, ameongeza kuwa mtu yeyote anaruhusiwa
kushiriki lakini asiwe chini ya miaka 18, ambapo mwaka huu shindano
hilo linadhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi Vodacom, Litah Paulsen
ameongeza kuwa Jaji machachari katika mashindano yaliyopita Salama
Jabir pamoja na kuwa kwa sasa yuko nje ya nchi lakini kwenye shindano la
mwaka huu pia atakuwepo na anatarajiwa kufanya kazi yake ya ujaji kama
ilivyokuwa katika shindano la miaka iliyopita, katika picha aliyeko
kushoto ni George Rwehumbiza meneja udhamini na mawasiliano wa kampuni
ya Vodacom
Friday, March 28, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment