Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide katika pozi na mume wake Gardner Habash ‘Kapteini’ .
Akizungumza
na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye mgahawa
wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar
mwishoni mwa wiki iliyopita, Jide alisema kuwa yeye na Gardner
wamefikia hatua ya kuishi katika staili hiyo kutokana na mapenzi yao
yaliyopitiliza.“Gardner ananipenda sana na mimi pia vilevile nampenda sana mume wangu. Mapenzi yetu yamepitiliza hadi tunajiona kama vile tumezaliwa tumbo moja na ndiyo maana nawaambia kuwa mimi na yeye tunaishi kama kaka na dada,” alifunguka Jide.
Akiendelea kuzungumza kwa kujiamini, Jide alisema kuwa hadi simu ya mkononi wanatumia moja kwa ajili ya mawasiliano.“Mimi hapa sina simu, anayo mume wangu lakini wakati mwingine nakuwa nayo mimi ila muda mwingi anakuwa nayo Gardner,” alimalizia Jide.
-GP
RSS Feed
Twitter
7:31 AM
Unknown
Posted in
0 comments:
Post a Comment