Tayari
staa huyo wa Tupogo ameshawaonesha mashabiki wake baadhi ya picha za
uchukuaji wa video hiyo iliyoongozwa na Mnaijeria aishiye London,
Uingereza, Moe Musa zikiwemo zile anazoonekana akiwa chini ya ulinzi wa
polisi.
Muongozaji
huyo wa video leo ameshare picha nyingine inayoonesha akiwa kwenye
mchakato wa kuhariri video hiyo na tumegundua kitu kingine- Ommy alikufa
kwenye video hiyo.. patamu hapo (kwa sauti ya Soudy Brown).
Katika
picha hiyo, Ommy Dimpoz anaonekana akiwa kwenye jeneza. “Color
Grading/Correcting @ommydimpoz Music Video. Visuals look #Frosh2Death,”
ameandika muongozaji huyo.
Hivi
karibuni, Ommy Dimpoz alisema kabla hata ya kufahamu kuwa Sofia
Skvortsova ndiye model atakayemtumia kwenye video yake, alikuwa amemuona
na akatamani msichana kama yeye aonekane kwenye video hiyo.
“Kwanza
yule msichana wakati mimi natoka naelekea location, tupo kwenye taa
hivi ambapo tunavuka taa ambazo ukizivuka unaelekea eneo la location
nikawa namuona msichana yaani mzuri halafu nikawa nasema kimoyomoyo
kwasababu nilikuwa sijamuona nikakutana naye location moja kwa moja,
hatukukutana siku ya kwanza tukapanda, hapana, alikuja moja kwa moja
siku ya kushoot,” Ommy aliiambia Xdeejayz.
Alisema
baada ya kumuona Sofia alimwambia mshkaji wake kuwa anatamani msichana
kama huyo awe kwenye video yake. Ameongeza kuwa siku ya kufanya video
alipofika location akamkuta Sofia eneo hilo na kumchanganya zaidi Ommy.
“Baadaye
Moe Musa ndio ananiita ananitambulisha ‘huyu ndio video model, sijui
unamuonaje,” ameelezea Ommy. “Mimi nikamwambia, ‘mimi nimempenda sana’
mimi nilimuambia nataka msichana mzuri kulingana na uzuri wa nyimbo na
maadhui ya nyimbo yalihitaji msichana mzuri.”
Ommy
alida kuwa kama mambo yakienda sawa anafikiria kumleta Sofia Tanzania
siku ya uzinduzi wa video hiyo. Tangu amtambulishe kwenye Instagram,
Sofia amepata followers wengi kutoka Tanzania. “Alipata followers wengi
kutoka huku kwahiyo akashangaa sana halafu akaappreciate.”
VIA xdeejayz
0 comments:
Post a Comment