Wednesday, May 7, 2014

 


Msanii chipukizi wa bongo fleva Walter Chilambo leo amefunguka baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu toka msanii wa hip hop Ney wa mitego kumponda katika wimbo wake wa salamu zao. Walter ni msanii huyo ambaye ni zao la bongo star search alikumbana na rungu la Ney baada ya Ney kuona msanii huyo hana kitu ingawa alipewa Tsh. milioni hamsini.

Katika kumjibu Ney, Walter  aliyekuwa akihojiwa na azam Tv 2 alisema yeye hana kinyongo wala bifu na Ney kwa kuchanwa katika wimbo huo. Kwanza anashukuru kwa Ney kumuimba kwani kumemuongezea yeye Walter umaarufu.

Pia Walter amesema si kweli kwamba hakupewa pesa za ushindi, pesa alipewa na amefanyia mambo ya maendeleo yeye na familia yake. Aliendelea kusema kwamba watu wengi walitegemea wamuone anajichanganya kama mastaa wengine kwenye kumbi za starehe lakini yeye hayupo hivyo.

Alimalizia kwa kusema ana ndoto za kushirikiana na wanamuziki wa kimataifa ili kujitangaza zaidi.

0 comments:

Post a Comment