Mama
yake na marehemu Hussein Mkieti aka ‘Sharo Milionea’ .Makubwa! Mama
mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu na muziki, marehemu Hussein Mkieti
‘Sharo Milionea’ amemtuhumu msanii wa vichekesho ambaye alikuwa rafiki
wa mwanaye, Musa Kitale kuwa alikula michango ya kumbukumbu ya kifo cha mwanaye, mwaka jana.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, Mama Sharo amekuwa akimlalamikia Kitale kwa
watu kwamba alikula fedha za mchango wa mwanaye hivyo kupigwa marufuku
kwamba kitu chochote kinachomhusu Sharo asipewe.
Ilidaiwa
kwamba, chanzo cha mama Sharo kutaka Kitale asipewe kitu chochote
kinachomhusu marehemu ni baada ya hivi karibuni Klabu ya Bongo Movie
Unity kutangaza kuwa litatoa Tuzo kwa Sharo Milionea kama kumbukumbu
kwani alikuwa ni mwenzao katika tasnia ya filamu.
Ilisemekana kuwa
mama huyo alielezwa kwamba tuzo hiyo itapokelewa na Kitale ndipo
alipokataa na kusema hataki kabisa kitu chochote kipitie kwa msanii huyo
kwa sababu huwa hamfikishii.
Msanii
wa vichekesho Musa Kitale.“Mama Sharo amekuwa akilalamika kwa muda
mrefu sana kwamba Kitale anatumia vitu vya mwanaye, eti alichangisha
michango ya kumbukumbu hakumfikishia hivyo kwa sasa ameamua kupiga
marufuku asikabidhiwe kitu chochote,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya
kupata habari hizo, wanahabari wetu walimtafuta Kitale ambapo kabla
hata ya kujibu tuhuma hizo, alinyanyua simu na kumpigia mama Sharo
kumuuliza kama kweli amezungumza madai hayo.
Mama Sharo alikiri kuwa
ni kweli alizungumza akidai alifikia uamuzi huo baada ya kutonywa na
watu kuwa Kitale amekuwa ‘akichikichia’ fedha za marehemu mwanaye.
Kitale,
baada ya kujiridhisha, alitoa ufafanuzi kuwa madai hayo hayana ukweli
na kudadavua kwamba wakati wa kumbukumbu ya Sharo mwaka mmoja (Novemba)
tangu alipofariki dunia, hakuna michango yoyote iliyotolewa.
“Inaniuma
sana kwa sababu enzi za uhai wa Sharo hatukuwahi kugombana hata siku
moja na mama Sharo alikuwa analitambua hilo, tuliishi kama ndugu na mimi
ndiye niliyemsaidia mpaka akapata umaarufu lakini sasa namshangaa huyu
mama kunishutumu vitu vya uongo,” alisema Kitale kwa huzuni huku jasho
likimtiririka.
source: kiuyahaki blog
0 comments:
Post a Comment